Na Mwandishi Wetu
Baraza la Madiwani Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo January 30, 2023 limejadili na kupitisha rasimu ya bajeti kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 kiasi cha fedha za Kitanzania Billion 38.9
Baraza hilo limefanyika katika Ukumbi wa Manispaa hiyo ikiwa ni Mkutano maalumu wa kupitia na kujadili rasimu ya mpango wa bajeti
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 inatarajia kukusanya jumla ya fedha za Kitanzania billion 38.9 , Mapato ya ndani ikikusanya fedha za Kitanzania billion 3.6 , fedha za ruzuku kutoka Serikali Kuu billion 23.9 na fedha za miradi ya maendeleo ikiwa ni billion 10.5
Rasimu ya bajeti hiyo imeongezeka kutoka billion 38.0 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 hadi kufikia billion 38.9 kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 sawa na ongezeko la Milion 943.7 ambayo ni 2.48% ongezeko hilo ni kutokana na kuongezeka kwa makisio ya fedha za miradi ya Maendeleo
Rasimu ya mpango na bajeti iliyopitishwa kwa Mwaka 2023/2024 imeandaliwa kwa kuzingatia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020- 2025, Malengo ya maendeleo endelevu (SDGs), Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Taifa 2025 , Sheria ya Bajeti Na. 11 ya Mwaka 2015 sura ya 349, Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (05) 2021- 2026,
Miongozo mingine iliyozingatiwa ni pamoja na Mipango shirikishi ya Jamii kwa kutumia dhana ya fursa na vikwazo kwa Maendeleo (O & OD) iliyoboreshwa, Mpango mkakati wa Halmashauri 2021/2022 -2025/2026, Mwongozo wa bajeti kwa Mwaka wa fedha 2023/2024, Maelekezo na ahadi mbalimbali za Viongozi Wakuu wa Kitaifa na Maazimio mbalimbali ya vikao vya Halmashauri
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa