Na Mwandishi Wetu
Wajumbe wa Kamati ya Wakuu wa idara na Vitengo (CMT) Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo April 02, 2024 wamefanya ziara ya kukagua na Kutembelea Ujenzi unaoendelea katika Hospitali ya Manispaa hiyo.
Ziara hiyo imefanyika ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bi. Mwantum Mgonja ambapo pia Wamekagua huduma za Matibabu zinazoendelea kutolewa kwa wagonjwa wa nje.
Hospitali ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji iliyopo Kata ya Kagera ilizinduliwa Februari 19, 2024 kwa lengo la kuanza kutoa huduma za Matibabu kwa Wagonjwa wa nje (OPD), Mapumziko ya mda mfupi kwa Wagonjwa waliozidiwa na vipimo vya maabara.
Kwa sasa jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) limekamilika na linatumika huku jengo la Maabara, Jengo la Wazazi (Maternity Complex), Jengo la mionzi, na Stoo ya dawa ujenzi ukiendelea.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa