Na Mwandishi Wetu
Watumishi wa Kada mbalimbali Manispaa ya Kigoma/Ujiji Jana July 24, 2024 walikutana katika ukumbi wa Manispaa hiyo kwa lengo la kujadili changamoto za kiutumishi.
Kikao hicho kilifanyika kikiongozwa na Mbunge wa Viti Maalimu anayewakilisha kundi la Wafanyakazi Katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Alice Karungi Kajage.
Aidha Watumishi hao walijadiliana masuala ya Kiutumishi yakiwemo Miundo ya kiutumishi, Stahiki na Mishahara, Likizo, Uhamisho na utoaji huduma kwa Wananchi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi wa vyama vya Wafanyakazi na uongozi wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi Mkoani Kigoma.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa