Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amewataka Wahudumu wa afya katika kituo cha afya cha Ujiji kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia misingi na maadili ya kazi.
Ameyasema hayo Leo August 21, 2024 alipofanya ziara katika kituo hicho na kufanya kikao na Wahudumu wa afya kwa lengo la kuwasimamia na kuwakumbusha Wajibu walio nao kwa jamii.
Amesema katika kituo hicho kumekuwa na malalamiko ya baadhi ya Wananchi kwa namna Wahudumu wa afya wanavyotekeleza majukumu yao huku akiwataka kubadilika katika utendaji na kuahidi kuchukua hatua za kinadhamu kwa ambao hawatabadilika.
Aidha amewataka kufanya kazi kwa weredi, kutumia lugha safi, kutumia mifumo ya kielekroniki katika matibabu na malipo ambapo pia alihitimisha kwa kukagua miundombinu ya kituo ikiwa ni pamoja na kuwajulia hali baadhi ya Wagonjwa Waliokuwa wakiendelea na matibabu.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa