Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba ameendelea kuwasisitiza wafanyabiashara kuendelea kulipa tozo na kodi kwa hiari pasipo kaguzi kwa maendeleo ya Manispaa hiyo.
Ameyasema hayo Leo Septemba 10, 2024 alipofanya kikao na Wamiliki wa nyumba za kulala Wageni katika Ukumbi wa Manispaa.
Mkurugenzi huyo amesema Manispaa imeendelea kuboresha mazingira ya Wafanyabiashara wa nyumba za kulala Wageni pasipo kutumia kaguzi ili kuepuka usumbufu kwa Wateja na mianya ya rushwa kwa Wamiliki.
Aidha amewataka Wamiliki wa nyumba za kulala Wageni kuendelea kuwasilisha vitabu kwa wakati, Kikao hicho ni cha pili kwa kundi hilo la Wafanyabiashara hao ambapo kikao cha kwanza Mkurugenzi huyo alisitisha kaguzi katika nyumba za kulala Wageni katika ukusanyaji mapato.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa