Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kigoma Leo May 10, 2023 imefanya ziara ya kukagua njia na miradi inayotarajiwa kutembelewa na Mwenge wa uhuru Mwaka huu
Ziara hiyo imefanyika ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu. Salumu Hamis kali ambapo kiongozi huyo akiwa kwenye ziara ametoa maelekezo kwa Wakurugenzi kuhakikisha wanapima na kupata hati miliki maeneo yanayomilikiwa na Serikali
Katika ziara hiyo miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na eneo la Mapokezi, Mkesha, miradi ya Elimu, Afya, Maji na Miundombinu ya barabara
Mwenge wa uhuru unatarajiwa kupokelewa Mkoani Kigoma Agusti 08, Mwaka huu na Manispaa ya Kigoma/Ujiji kupokelewa Augusti 16, na Kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Tunza mazingira, Okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai, na Uchumi wa Taifa"
Zaidi www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa