Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeibuka mshindi wa tuzo na kuwa mshindi wa pili katika kundi la Halmashauri katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane Nane )kanda ya Magharibi yaliyofugwa Leo August 8, 2022 katika viwanja vya Nane Nane eneo la Ipuli Manispaa ya Tabora huku Manispaa ya Tabora ikiibuka Mshindi wa Kwanza
Akikabidhi Kombe na Cheti cha Ushindi Mgeni Rasmi ambaye amekufunga maonesho hayo kwa Mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Adengenye ameipongeza Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kuleta Wakulima , Wafugaji na Wajasiriamali waliopelekea Manispaa hiyo kuibuka Mshindi kutokana na mazao na bidhaa walizozionesha ikiwa ni pamoja na Teknolojia na Ubunifu
Aidha amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe kwa kazi anayoifanya katika kushirikiana na Wananchi wa Wilaya ya Kigoma katika kutekeleza miradi ya Maendeleo huku akiipongeza pia Manispaa ya Kigoma/Ujiji chini ya Waheshimiwa Madiwani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo
Jumla ya Halmashauri kumi na sita (16) za Mkoa wa Kigoma na Tabora zimeshiriki Maonesho hayo huku mshindi wa tatu akiwa ni Halmashauri ya Kaliua iliyopo Mkoani Tabora
Katika banda la Manispaa ya Kigoma/Ujiji Wakulima, Wafugaji , na Wajasiriamali walioshiriki katika maonesho hayo walikuwa na bidhaa kama vile Samaki wanaovuliwa Ziwa Tanganyika (Maarufu kwa jina la Mgebuka), Dagaa, Uchakataji, Usindikaji na Ufungaji wa Mafuta ya Mawese, Sanaa za Uchongaji, biashara ya Vitenge na Mashuka ya kufuma (Maarufu Mashuka ya Kigoma), Bidhaa za Viungo, na Unga wa Mhogo
Aidha Teknolojia iliyooneshwa ni ni pamoja na Teknolojia ya Uzalishaji wa Miche ya Michikichi ya Kisasa aina ya Tenera, Teknolojia ya Ufugaji wa Samaki na Samaki wa Mapambo, Kilimo cha Nyanya na Mahindi
Kauli Mbiu ya Mwaka huu kwa Sikukuu ya Wakulima na Wafugaji (Nane Nane) ni " Agenda 10/30: Kilimo ni Biashara, Shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".
Karibu Banda la Manispaa ya Kigoma/Ujiji katika maonesho yajayo mwaka 2023.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa