Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Novemba 20, 2024 imekabidhi eneo la Ujenzi wa Soko Kisasa la Mwanga na Mwalo wa Katonga kwa uongozi wa Kampuni ya ujenzi ya ASABHI CONTRACTOR LIMITED kwa kushirikiana na PIONEER BUILDERS LIMITED.
Makabidhiano yamefanyika na timu ya Menejimenti ya Wakuu wa idara na vitengo wa Manispaa wakiongozwa na Mkurugenzi Ndugu. Kisena Mabuba kwa kuonesha mipaka na ramani ya eneo la ujenzi.
Mkurugenzi huyo amesisitiza Mkandarasi mjenzi kuhakikisha anatoa ajira kwa Wakazi na Wazawa wa Manispaa huku akizingatia usalama wa wafanyakazi na Wananchi kwa kuweka alama za usalama ikiwa ni pamoja na udhibiti wa taka.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/ Ujiji ilisaini Mkataba wa ujenzi wa Soko Kisasa la Mwanga na Mwalo wa Katonga na Kampuni ya ujenzi Novemba 02, Mwaka huu kwa gharama ya fedha za Kitanzania zaidi ya Billioni kumi na Sita (Tsh 16, 495, 359, 710. 275/=).
Miradi hii inatekelezwa kwa mda wa miezi kumi na mbili (12) kuanzia Novemba 15, 2024 hadi Novemba 14, 2025 ambapo utakuwa umekamilika.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa