Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/ Ujiji imesaini Mkataba wa ujenzi wa Soko Kisasa la Mwanga na Mwalo wa Katonga na Kampuni ya ujenzi ya ASABHI CONTRACTOT LIMITED kwa kushirikiana na PIONEER BUILDERS LIMITED kwa gharama ya fedha za Kitanzania zaidi ya Billioni kumi na Sita (Tsh 16, 495, 359, 710. 275/=).
Mkataba huo umesainiwa Kati ya Viongozi wa kampuni ya ujenzi na Viongozi wa Halmashauri Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mhe. Baraka Naibuha Lupoli na Mkurugenzi wa Manispaa Ndugu. Kisena Mabuba
Aidha utiaji saini umeshuhudiwa na Mgeni rasmi Naibu Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba, Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa taasisi, Wananchi na Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Miradi hii inatekelezwa kwa mda wa miezi kumi na mbili (12) kuanzia Novemba 15, 2024 hadi Novemba 14, 2025 ambapo utakuwa umekamilika.
Akihutubia Wananchi Naibu waziri wa Tamisemi Mhe. Zainab Katimba amewataka viongozi kusimamia utekelezaji kikamilifu na Wananchi kutunza miundombinu inayotekelezwa.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa