Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba Jana August 21, 2024 alikutana na kufanya kikao na baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kitaifa wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF).
Kikao kilifanyika ukumbi wa Manispaa hiyo ambapo kiongozi huyo aliwataka fedha wanazozipata kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kujiinua kiuchumi kwa kufanya shughuli za uzalishaji mali.
Alisema Serikali inaendelea kutoa elimu kwa Wanufaika hao namna ambavyo fedha wanazozipokea zinaweza kuwanufaisha kupata mahitaji ya Msingi na Katika kushiriki shughuli za kiuchumi.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa