Na Mwandishi Wetu
Wataalamu mbalimbali kutoka ngazi za Mkoa na Halmashauri kutoka Mikoa ya Kigoma na Kagera Leo Desemba 22, 2022 Wamekutana katika mafunzo ya siku mbili (02) katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kasulu kwa lengo la kuzijengea timu za utekelezaji wa mradi mpya wa BOOST
Wataalamu hao Waliohudhuria mafunzo hayo ni pamoja na Maafisa elimu, Walimu wakuu, Waratibu elimu Kata, Wahandisi, Maafisa Maendeleo ya jamii, Wahasibu, Maafisa mipango na Uchumi, Maafisa Manunuzi, Wadhibiti ubora wa elimu pamoja na Maafisa Mawasiliano Serikalini
Mgeni rasmi wa Mafunzo hayo ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi idara ya elimu Mkoa wa Kigoma Bi. Paulina NdigezĂ akihutubia Washiriki wa mafunzo hayo amewataka kuzingatia mafunzo hayo kwa lengo la kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa ufanisi
Awali Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka OR-TAMISEMI Ndugu. George Jackson Mbijima amesema mradi wa BOOST unatarajiwa kutekelezwa kwa mda wa miaka mitano (05) kwa Mwaka 2021/2022 hadi Mwaka 2025/2026 kwa fedha za Kitanzania Trillion 1. 15 sawa na Dora za Kimarekani Million Mia tano
Amesema katika fedha hizo Dola za Kimarekani Million 480 zitatumika katika program ya lipa kulingana na matokeo na Dola za Kimarekani Million 20 ni gharama za utekelezaji wa uwekezaji wa miradi
Ameendelea kusema katika Mradi huo jumla ya vyumba vya Madarasa 12, 0000 vinatarajia kujengwa, ununuzi wa vifaa vya kisasa vya Tehama kwenye Shule zaidi ya mia nane (800) za Msingi na Vituo vya Walimu, na uandaaji wa vifaa vya kufundishia na Kujifunzia kwa elimu ya awali
Aidha malengo mengine ya mradi ni kuongeza uandikishaji wa elimu ya awali kutoka 76.9% mwaka 2021 hadi zaidi ya 85%, mafunzo endelevu ya Walimu kazini (MEWAKA), na Halmashauri kusimamia utawala bora katika elimu kwa kuzingatia miongozo na usimamizi wa Shule
Amehitimisha kwa kusema Shule za Msingi 6,000 zitateleleza mradi wa programu ya Shule ya Msingi Salama na kufanya Wanafunzi 50% wa darasa la pili kufikia kiwango cha chini cha kumudu stadi za Kusoma na kuandika na 35% katika kuhesabu
Mradi wa BOOST tayari Umeanza kutekelezwa Nchini Tanzania kwa Mikoa ya Tanzania bara kwa kutoa mafunzo mbalimbali na utambulishaji wa mradi na unatarajia kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa