• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kigoma Ujiji Municipal Council
Kigoma Ujiji Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango,Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha nyuki
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Sekta ya Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha Ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati Za Kudumu Za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Ukimwi
      • Kamati Ya Maadili
      • Uchumi Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Kamati Za Madiwani
      • Ratiba Kuonana Na Meya
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyo Kamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba
    • Picha za Kuona
      • Mh.Meya
    • Tukio
    • Habari

"RAIS DR. SAMIA AMEITENDEA HAKI KIGOMA" DC KIGOMA Congraturation

Posted on: April 15th, 2024

Na Mwandishi Wetu

 Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Kali ameeleza miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita huku akimshukuru Rais Dr.  Samia Suluhu Hassani kwa namna ambavyo amewezesha fedha za miradi katika Wilaya hiyo.

Pongezi na Shukrani hizo amezitoa leo April 15, 2024 katika Kikao kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo kilichofanyikia katika Ukumbi wa Kanisa la Angrikani uliopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji.


Kikao kazi hicho kimehusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi, Wakuu wa idara na Vitengo, Watendaji wa Kata, Waratibu elimu Kata,  Wakuu wa Shule, Wenyeviti wa Mitaa,Vijiji na Vitongoji kutoka Halmashauri zote mbili  Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.


Katika Kikao kazi hicho amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassani imeitendea haki Mkoa na Wilaya za Kigoma, ambapo katika Wilaya hiyo imetekeleza na inandelea kutekeleza Ujenzi wa Meli Mpya Mkoani Kigoma kwa gharama Tsh Billion 322/=, Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Uhasibu (TIA) unaoendelea kwa gharama ya Tsh Billion 37/=, na Ujenzi wa Bandari ya Kibirizi na Ujiji  kwa gharama ya Tsh Billion 37/=.


Miradi mingine aliyoitaja ni pamoja na Ujenzi wa Reli ya Kisasa(SGR) kipande kutoka Kigoma hadi Tabora kwa gharama ya Tsh Trioni 6/=, Ujenzi wa Hospitali mbili (02) unaoendelea Manispaa ya Kigoma Ujiji naHalmashauri ya Wilaya ya Kigoma.


Miradi mingine ni ya kupitia mradi wa TACTICS ambayo ni pamoja na Ujenzi wa Barabara ya Wafipa-Kagera yenye urefu wa Km 2.434, Daraja la Mto Ruiche, Ujenzi wa barabara ya Bangwe-Burega- Ujiji yenye urefu wa Km 7.1, Ujenzi wa mitaro ya kutiririsha maji ya Mvua katika maeneo ya Bangwe,  Burega,  Rutale,  Mlole , Bushabani, Mji mwema,  na Katonyanga yenye urefu Km 5.288, Ujenzi wa Kisasa soko  la Mwanga, Ujenzi wa Kisasa wa Soko la mazao ya Uvuvi Katonga, na Ujenzi wa barabara ya Old Kasulu yenye urefu wa Km 7.


Aidha amewataka Viongozi waliohudhuria Kikao kazi hicho kuendelea kusimamia Suala la Ulinzi katika maeneo yao kwa kutoa taarifa za Wahamiaji haramu,  Wananchi kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha Mvua,  Usafi wa Mazingira pamoja na kusimamia ukusanyaji wa mapato.


Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz  



Matangazo

  • NYARAKA ZA WAKUU WA SHULE WALIMU WAKUU October 10, 2022
  • Ufatiliaji wa Kina Kusaka wasiokata Leseni za Biashara 2017 March 20, 2017
  • Fedha za Mradi wa P4R mwezi Machi 2017 April 13, 2017
  • Fedha za Mradi wa Barabara Machi 2017 April 13, 2017
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • NYUMBA YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MJIMWEMA IPO HATUA YA UMALIZIAJI. Building

    May 08, 2025
  • MAANDALIZI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU YAENDELEA UJIJI, DC AKAGUA MIRADI. National touch

    May 07, 2025
  • SERIKALI YAENDELEA KUTOA MSAADA WA KIBINADAMU WAATHIRIKA WA MVUA KIGOMA UJIJI. Flood

    May 05, 2025
  • NMB YAKABIDHI VIFAA TIBA KIGOMA UJIJI. Health

    May 03, 2025
  • Angalia Yote

Picha za Kuona

MWENGE WA UHURU 2023
Picha za Kuona Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Ofisi ya Rais Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tume ya Ajira

Kurasa Husishi

  • Wizara ya Elimu
  • Wizara ya Afya
  • TCU
  • Mikopo Vyuo Vya Elimu Ya Juu
  • Ofisi ya RAS Kigoma
  • Jiji Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Manispaa ya Kigoma Ujiji

    Sanduku la Posta: S.L.P 44

    Simu: +255 28 2802535

    Namba ya Simu: +255765660847

    Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz

Mawasiliano Mbalimbali

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa