Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amekabidhi Gari moja (01) na Pikipiki kumi na mbili (12) kwa Halmashauri nane (08) za Mkoa kwa lengo la usambazaji wa chanjo huku akiwataka Wakuu wa Wilaya kusimamia vyombo hivyo vya moto ili kufanya kazi iliyokusudiwa na kwa ufanisi.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashidi Chuachua kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya Leo Januari 28, 2025 ambapo Mkuu huyo wa Mkoa ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo imekuwa ikiboresha miundombinu katika sekta ya afya Mkoani hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua ameendelea kuishukuru Serikali huku akisema vifaa hivyo vitasimamiwa na kufanya kazi iliyokusudiwa kwa utoaji wa elimu na usambazaji chanjo ili kulinda afya za Wananchi wa Mkoa huo.
Awali akizungumza Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Damas Kayera amesema gari hilo litatumika kusambaza chanjo kwa Wilaya za Mkoa huo huku kila halmashauri ikipata pikipiki 1 na pikipiki nne (04) zikigawiwa katika vituo vya afya vya Lukoma, Mwamgongo, Kibuye na Kinazi ili huduma hizo kutolewa kwa haraka.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa