Na Mwandishi Wetu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Hassan Rugwa amewataka Watumishi wa Serikali kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo kwa ufanisi pamoja na kusikiliza na kutatua kero za Wananchi katika maeneo yao.
Ameyasema hayo Leo April 15, 2024 katika Kikao kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salumu Kali kilichofanyikia Ukumbi wa Kanisa la Angrikani uliopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Katibu Tawala amewataka Viongozi hao kuwa na utamaduni wa kutoa taarifa kwa Wananchi juu ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na kueleza mafanikio ya Serikali katika maeneo wanayosimamia.
Kikao kazi hicho kimehusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi, Wakuu wa idara na Vitengo, Watendaji wa Kata, Waratibu elimu Kata, Wakuu wa Shule, Wenyeviti wa Mitaa,Vijiji na Vitongoji kutoka Halmashauri zote mbili Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa