Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja amewataka Watumishi wa kituo cha afya cha Ujiji kutoa huduma bora za Matibabu kwa Wananchi na Wakazi wa Manispaa hiyo
Ameyasema hayo Leo Septemba 13, 2023 alipofanya kikao na Watumishi wa kituo hicho kwa lengo la kuongeza tija na ufanisi katika utoaji wa huduma za matibabu
Mkurugenzi huyo amewataka Watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu, Kanuni na sheria ikiwemo Maadili ya kazi kwa kutosababisha Upotevu wa dawa, kulinda mali za Serikali, na kufika kazini kwa wakati,
Kikao hicho kimehudhuliwa na Mganga Mkuu wa Manispaa, Timu ya usimamizi wa uendeshaji huduma za afya Manispaa (CHMT), Madaktari wa Kituo, Wauguzi, Wafamasia, Wataalamu wa Maabara, Madereva na Walinzi wa Kituo cha afya cha Ujiji
www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa