• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kigoma Ujiji Municipal Council
Kigoma Ujiji Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Rasilimali Watu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango,Takwimu na Usimamizi
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha nyuki
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Sekta ya Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha Ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati Za Kudumu Za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Ukimwi
      • Kamati Ya Maadili
      • Uchumi Afya na Elimu
    • Ratiba
      • Kamati Za Madiwani
      • Ratiba Kuonana Na Meya
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyo Kamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba
    • Picha za Kuona
      • Mh.Meya
    • Tukio
    • Habari

WAANDISHI WA HABARI MKOANI KIGOMA KUHAMASISHA ELIMU BORA KWA WOTE Education

Posted on: January 17th, 2023

Na Mwandishi Wetu

Wamiliki wa  vyombo vya habari na waandishi wa habari Mkoani Kigoma wametakiwa kushirikiana na Jamii katika kukuza Viwango vya elimu Mkoani hapo

Wadau hao wa habari wametakiwa na Katibu Tawala Msaidizi idara ya elimu Mkoa wa Kigoma  Bi. Paulina NdigezĂ   akimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa  huo Jana  January 16, 2023 katika kikao kilichofanyikia Ukumbi wa Hoteli ya Glonency uliopo Halmashauri ya Mji Kasulu  

Kikao hicho kilihusisha Wamiliki wa Vyombo vya habari, Maafisa Mawasiliano Serikalini, Maafisa elimu ngazi ya Mkoa , na Waandishi wa Habari waliopo Mkoani hapo

Katika kikao hicho kiongozi huyo aliwataka wadau hao wa vyombo vya habari kuendelea kutoa taarifa na elimu kwa umma juu ya miradi inayotekelezwa Mkoani hapo ikiwemo mradi wa Shule Bora

Aliendelea  kuwataka kuelimisha jamii kushiriki kwa kuzifanya Shule ziwajibike na kuongeza uelewa wa Jamii kuhusu umuhimu wa kila Mtoto( Kike au Kiume), na Watoto  wenye ulemavu kuandikisha na kuhudhuria Shule

Awali akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji Afisa habari wa Mradi wa Shule Bora Ndugu. Raymond kayombo alisema mradi wa Shule bora umekuwa ukitekeleza mafunzo ya Walimu kazini (MEWAKA) kwa lengo la kuboresha suala la  Ufundishaji na Ujifunzaji

Aidha amesema tayari Maafisa Mawasiliano Serikalini kwa ngazi ya Mikoa na Halmashauri inayotekeleza mradi wamefanya vikao na kuweka maazimio namna watakavyofanya kazi na Wamiliki wa vyombo vya habari pamoja na  Waandishi  wa Habari katika kuboresha utoaji wa taarifa za mafanikio

Alisema katika utekelezaji wa mradi wa Shule bora Wajibu wa Wamiliki wa vyombo vya habari na waandishi wa habari ni kuibua changamoto na uelimishaji wa jamii katika maeneo yanayotekelezwa na mradi ikiwemo suala la Ufundishaji , Mazingira salama ya kujifunzia, Elimu jumuishi, Ufaulu na Mdondoko wa wanafunzi

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais TAMISEMI  Ndugu. Fred Kibano aliwataka  Waandishi wa Habari  kutumia kalamu zao kufikisha ujumbe kwa jamii kupitia Uandishi wa Habari, makala,  uandaaji wa vipindi kupitia vyombo vyote vya habari ikiwemo magazaeti, radio, televisheni,  na mitandao ya kijamii ili kufikisha ujumbe kwa makundi mbalimbali  

Naye Mwenyekiti Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Kigoma Ndugu. Jackob Ruvilo alisema Waandishi wa habari wataendelea kushirikiana na Serikali kupitia Mradi wa Shule Bora  kuhabarisha na kuelimisha jamii kuhakikisha Watoto wanapata elimu bora kupitia Wadau mbalimbali wakiwemo Jamii, Wazazi, Walimu na Mamlaka zinazosimamia elimu Mkoani hapo  

Miradi wa Shule bora unatekelezwa katika Mikoa tisa (9) Nchini Tanzania ukihusisha Halmashauri sitini na saba (67) na Shule elfu tano  mia saba hamsini na saba   ( 5, 757) na Unatarajia kuwanufaisha Wanafunzi zaidi ya Milioni tatu na laki nane ( 3, 800,000) na Walimu zaidi ya  elfu hamsini na nne ( 54, 000)

Mikoa inayotekeleza mradi wa Shule bora ni pamoja na Mkoa wa Kigoma, Katavi, Dodoma, Mara, Pwani,  Rukwa, Simiyu, Singida na Mkoa wa Tanga

#shulebora

Matangazo

  • NYARAKA ZA WAKUU WA SHULE WALIMU WAKUU October 10, 2022
  • Ufatiliaji wa Kina Kusaka wasiokata Leseni za Biashara 2017 March 20, 2017
  • Fedha za Mradi wa P4R mwezi Machi 2017 April 13, 2017
  • Fedha za Mradi wa Barabara Machi 2017 April 13, 2017
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • NYUMBA YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MJIMWEMA IPO HATUA YA UMALIZIAJI. Building

    May 08, 2025
  • MAANDALIZI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU YAENDELEA UJIJI, DC AKAGUA MIRADI. National touch

    May 07, 2025
  • SERIKALI YAENDELEA KUTOA MSAADA WA KIBINADAMU WAATHIRIKA WA MVUA KIGOMA UJIJI. Flood

    May 05, 2025
  • NMB YAKABIDHI VIFAA TIBA KIGOMA UJIJI. Health

    May 03, 2025
  • Angalia Yote

Picha za Kuona

MWENGE WA UHURU 2023
Picha za Kuona Zaidi

Kurasa za Haraka

  • Ofisi ya Rais Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tume ya Ajira

Kurasa Husishi

  • Wizara ya Elimu
  • Wizara ya Afya
  • TCU
  • Mikopo Vyuo Vya Elimu Ya Juu
  • Ofisi ya RAS Kigoma
  • Jiji Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Manispaa ya Kigoma Ujiji

    Sanduku la Posta: S.L.P 44

    Simu: +255 28 2802535

    Namba ya Simu: +255765660847

    Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz

Mawasiliano Mbalimbali

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa