Na mwandishi wetu.
Waziri wa TAMISEMI Sulemani Jafo jana march 14 katika ukumbi wa NSSF uliopo manispaa ya Kigoma/Ujiji alizindua mfumo wa taarifa za kijiografia (GIS) uliofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa kimkakati wa ukuzaji wa miji na majiji Tanzania(TSCP).
Akihutubia katika ukumbi huo alisema mfumo huo utasaidia katika ukuzaji wa mapato kwa halmashauri na namna ya kuwahudumia wananchi waliopo katika Manispaa hiyo kutokana na mfumo huo kuwa na taarifa mbalimbali zitakazoanza kukusanya kutoka kwa makazi yote, biashara na huduma za jamii zilizopo katika eneo husika.
Alisema Manispaa ya Kigoma/Ujiji ndio imekuwa sehemu ya kuandalia mfumo huo ikiwa imepangwa kutumika katika halmashauri nane zinazopitiwa na mradi wa TSCP na kufadhiliwa na Benki ya Dunia huku akiwataka watendaji kujifunza Mfumo huo na kuhakikisha wataalamu wa Tehama waliopo katika halmashauri zote nane wanatoa ushirikiano katika mfumo huo.
Akiendelea kuhutubia aligusia suala la upotevu wa mapato kutokana na upotevu wa mashine za kukusanyia mapato(POS) huku akiasa halmashauri kuchukua hatua za kimaadili katika upotevu huo huku akiasa halmashauri katika tumiaji wa fedha mbichi ambazo zinakuwa hazijafata taratibu katika kufikia matumizi.
Naye Eng.Mussa Nati mhandisi na mtaalamu wa mfumo wa GIS kutoka Benki ya Dunia alisema mfumo huo tayari umeshaanza kutumika katika wilaya ya Kinondoni na umeleta tija katika ujenzi wa barabara namna ambavyo haikuwa tatizo la migogoro ya fidia kwa wakazi huku akieleza umeweza kukuza mapato katika wilaya hiyo huku akitoa rai mfumo huo kutumika vizuri na kuulinda kupitia wataalamu waliopo.
Naye meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Hussein Ruhava alishukuru kwa kuona uzinduzi huo kufanyika katika manispaa hiyo huku akisema ni heshima kubwa ambayo serikali imeitoa huku akiahidi kutoa ushirikiano na madiwani wote katika ukusanyaji wa mapato kutokana na mfumo huo na kuitaka serikali kuitazama zaidi manispaa hiyo kutokana na uwepo wa huduma duni zilizopo.
Naye mkuu wa wilaya ya Kigoma kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Ndugu. Akitoa salamu kutokana na mfumo huo alisema kupitia ofisi ya Mkuu wa mkoa itatoa ushirikiano kwa kusimamia na kuhimiza halmashuri kutumia mfumo huo kwa usahihi na bila kuingilia mfumo huo katika uhalifu.
Waziri huyo baada ya kumaliza mkutano huo katika ukumbi wa NSSF ambapo viongozi mbalimbali walihudhulia kutoka ofsi ya Mkuu wa mkoa, Wakuu wa wilaya zote za mkoani Kigoma, wakurugenzi wa Halmashauri, Meya wa manispaa ya Kigoma/Ujiji, Mkurugenzi wa Kigoma/Ujiji, Madiwani, wataalamu, wenyeviti wa mtaa pamoja na waandishi wa habari alifanya ziara katika eneo la Msimba lilopo dampo la taka la manispaa hiyo ambapo alitoa tamko kuanza kutumika kuanzia sasa.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa