Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Kalli Leo Novemba 10, 2023 amezindua Zahanati mpya ya Kamala- Bangwe iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la kuanza kutoa huduma za afya kwa Wananchi.
Akihutubia Wananchi katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya amewataka Wakazi wa eneo hilo kutunza miundombinu ya Zahanati na kuwataka Wahudumu wa afya kutumia lugha nzuri katika kuhudumia Wagonjwa
Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Baraka Naibuha Lupoli amesema Manispaa hiyo imelenga katika kusogeza huduma karibu na Wananchi kwa kutekeleza miradi ya Maendeleo ambapo kwa sasa wanakamilisha ujenzi wa Ofisi za Kata za Kisasa kwa kila Kata huku akisema mpango wa Ujenzi wa Zahanati ni kwa kila Kata
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja amesema Ujenzi wa Zahanati hiyo umegharimu kiasi cha fedha za Kitanzania zaidi ya Million Mia moja na sita (Tsh 106, 292, 060/=) na vifaa tiba vikigharimu kiasi cha Million hamsini (Tsh 50, 000, 000/=) fedha kutoka Serikali Kuu.
Amesema kwa kipindi cha uongozi wa Rais Dr. Samia Suluhu Hassani Manispaa hiyo imepokea Fedha za Kitanzania zaidi ya Tsh Billion 3.4/= katika utekelezaji wa miradi ya afya na ununuzi wa vifaa tiba
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Dr. Hashim Mvogogo amesema Zahanati hiyo inaanza kutoa huduma kwa Wagonjwa wa Nje (OPD), Maabara na huduma za Mama, Baba, na Mtoto (kliniki) ambapo pia vyumba vya mapumziko vipo katika jengo hilo.
Zaidi www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa