Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua Siku ya Ijumaa Agosti 15, 2025 alifanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni Maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Kiongozi huyo alifanya ziara akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, pamoja Wakuu wa Idara na Vitengo.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa Bweni Shule ya Sekondari Buronge, Ujenzi wa Zahanati ya Rubuga, Ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kasimbu, Ujenzi wa barabara ya Met na kukagua Shughuli za Kikundi cha Vijana cha umoja wa mafundi Seremala.
Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Kigoma/Ujiji unatarajiwa kukimbizwa Septemba 21, Mwaka huu.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz #mwengewauhuru #mwengewauhuru2025
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa