Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo August 29, 2025 imekutana na kufanya kikao na Viongozi wa vyombo vya habari vya vilivyopo katika Manispaa hiyo ikiwa ni Maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025.
Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya hamasa ya Mwenge wa Uhuru 2025 ambaye ni Afisa elimu wa Awali na Msingi Ndugu. Richard Mtauka kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa.
Katika kikao hicho Mwenyekiti huyo amewashirikisha Wadau hao katika kufanya hamasa na ushiriki wa Wananchi kuelekea mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazokimbizwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Septemba 21, Mwaka huu.
Viongozi waliohudhuria kikao hicho ni kutoka Radio joy, Main FM, Cicora radio, Shakina FM pamoja na Hidaya FM.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru Mwaka huu ni "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu".
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa