Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua ametangaza Jumamosi ya Kila wiki ni Siku ya usafi wa Mazingira kwa Wakazi na Wananchi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kuanzia Saa moja hadi Saa nne Asubuhi.
Tangazo hilo amelitoa Leo July 27, 2025 alipofanya kikao kilichohusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wakuu wa Taasisi, Watumishi wa Makao makuu Ofisi ya Manispaa, Watendaji wa Kata , Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Viongozi wa Wafanyabishara.
Amesema kila jumamosi Wananchi Wote watashiriki Usafi wa Mazingira katika maeneo yao ya makazi na Biashara na kuwataka Watendaji wa Serikali kusimamia zoezi hilo.
Aidha amewataka Wananchi kushiriki mbio za Mwenge wa uhuru zitakazokimbizwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Septemba 21, kwa kujitokeza eneo la Mapokezi Shule ya Sekondari Buronge, maeneo ya miradi na eneo la Mkesha Uwanja wa Mwanga community centre.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa