Na Mwandishi Wetu
Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Kigoma/Ujiji wamefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo katika Manispaa hiyo ikiwa ni Maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025.
Ziara hiyo imefanyika Leo Julai 17, kwa kutembelea Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari unaoendelea Kata ya Kipampa kwa gharama ya ya fedha za Kitanzania Million Mia sita na tatu (Tsh 603,000,000/=) fedha kutoka Serikali Kuu, Ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kasimbu kwa gharama ya Tsh 63, 676, 400/= fedha kutoka Mapato ya ndani.
Miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi unaoendelea wa Zahanati mpya Kata ya Rubuga kupitia mapato ya ndani kwa gharama ya fedha za Kitanzania Million Mia moja na thelathini mbili (Tsh 132,000,000/=) hadi kukamilika, Kikundi cha Vijana Cha Lukondo kilichopo Kata ya Buhanda kikizalisha Kinywaji cha Lukondo na Umoja wa mafundi Seremala Katubuka.
Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Kigoma/Ujiji unatarajiwa kukimbizwa Septemba 21 Mwaka huu huku Wananchi na Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Wakihamasishwa kushiriki.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz #mwengewauhuru #Nationaltouch #mwengewauhuru2025
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa