Na Mwandishi Wetu
Utoaji wa huduma ya vipimo vya mionzi imeanza kutolewa kwa Wagonjwa wanaofika kupata matibabu katika Hospitali ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji iliyopo Kata ya Kagera.
Akitoa taarifa ya Utoaji wa huduma hiyo Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Dr. Hashim Mvogogo amesema tayari vipimo kwa njia ya Mionzi imeanza kutolewa mara baada ya Mashine ya X ray na Ultra Sound kufungwa.
Amewataka Wananchi kufika hospitalini hapo kupata vipimo vya X-ray ya Kichwa, Miguu, tumbo, Mikono, kifua na mgongo na vipimo vya Utra sound vinatolewa kwa Watu wote wakiwemo wajawazito huku akisema baada ya vipimo mgonjwa atapata huduma za matibabu.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa