Na Mwandishi Wetu
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Waratibu wa Jumuia za Kujifunza (JzK) kutoka Halmashauri nane (08) za Mkoani Kigoma Leo June 25, 2025 wanahitimisha mafunzo ya siku tatu (03) ambayo yamefanyikia Shule ya Sekondari Mwandiga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Mafunzo hayo yanafanyika chini ya Mradi wa Shule bora unaofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa UK Aid kwa lengo la kubadilishana na kujengeana uzoefu katika stadi za Uongozi na usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji katika Jumuia za Kujifunza (JZK).
Akizungumza katika mafunzo hayo Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Mwalimu Ramadhani Thabiti Abdallah amesema Jumuia za Kujifunza (JzK) ni umoja wa Walimu na Shule katika maeneo yao katika kupitia na kujadili ufanisi wa ufundishaji ikijumuisha kujadili mada tata.
Amesema mafunzo hayo yamewakutanisha Walimu Wakuu Hamsini na nne (54) wa Shule za Msingi kutoka Halmashauri nane (08)za Mkoa wa Kigoma ambapo wamejadiliana na kujengeana katika Utekelezaji wa jumuia za kujifunza (JzK), Uongozi na usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji, Dira, dhima na misingi ya Maadili ya Shule.
Manispaa ya Kigoma/Ujiji ina Jumuia za Kujifunza (JzK) Tano (05) ambazo ni Kabingo, Mwanga, Kigoma Bangwe, Dr. Living stone, na Ujiji.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa