Na Mwandishi Wetu
Kongamano la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's) Wilaya ya Kigoma lilifanyika Jana Juni 23, 2025 Manispaa ya Kigoma/Ujiji katika ukumbi wa Red Cross.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Afisa Tarafa Ndugu. Maximilian Cyrilo alipongeza mashirika yasiyo ya kiserikali kwa namna ambavyo yamekuwa yakiunga jitihada za Serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za jamii katika sekta mbalimbali.
Aliyataka mashirika kuendelea kutekeleza miradi yao kwa uwazi kwa kuendelea kutoa taarifa kwa Wananchi katika maeneo wanayotekeleza ikiwa ni pamoja na kufuata kanuni, taratibu na Sheria za Nchi.
Kauli mbiu ya kongamano ni “Tathmini ya Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa 2020/2021 – 2024/2025: Mafanikio, Changamoto, Fursa na Matarajio, ikiwa ni ishara ya dhamira ya pamoja kuimarisha Sekta ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini".
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa