Na Mwandishi Wetu
Ujenzi wa Bweni Shule ya Sekondari Buronge unaendelea ukiwa umefikia hatua ya upauaji kwa gharama ya fedha za Kitanzania Millioni Mia Moja thelathini na Sita (Tsh 136,000,000/=) fedha kutoka Serikali Kuu.
Kukamilika kwake litakuwa na uwezo wa kuchukua Wanafunzi themanini (80) na kufanya Ongezeko la Bweni katika Shule hiyo la Wasichana na Wavulana kwa Wanafunzi wa Kidato cha tano na sita.
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan imeendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili Wanafunzi wa Kitanzania wapate elimu bora katika mazingira rafiki na salama.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz. @ikulu_mawasiliano @msemajimkuuwaserikali @mabuba_fkm
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa