Na Mwandishi Wetu
Ubainishaji wa Wanafunzi wenye mahitaji maalumu unalenga kuboresha mbinu za Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Wanafunzi na Walimu.
Hayo yamebainishwa katika mafunzo yaliyofanyika Leo June 24, 2025 Shule ya Msingi Airport iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji yakitolewa na Timu ya ubainishaji wa Wanafunzi wenye mahitaji maalumu ngazi ya Halmashauri chini ya Mradi wa Shule bora unafadhiliwa na Serikali ya Uingereza Kupitia Mfuko wa UK aid.
Mwezeshaji wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Afisa elimu Kata, Kata ya Kagera Ndugu. Salvatory Meshack amesema mafunzo hayo yanalenga kuboresha mbinu za Ufundishaji na Mwanafunzi kuhudumiwa kwa kuzingatia mahitaji aliyonayo.
Amesema mafunzo hayo yanawajengea uwezo Walimu katika kuleta usawa katika kujifunza, kuepuka unyanyapaa na ukatili kutokana na hali ya Mwanafunzi kama vile Yatima, Viziwi, Albino, ulemavu wa viungo, Usonji, wenye Vipawa na vipaji.
Mafunzo hayo yametolewa kwa Maafisa elimu Kata na Walimu Wakuu wa Shule za Awali na Msingi katika Kata ya Katubuka, Buhanda na Businde.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz #shulebora
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa