TARATIBU ZA UHAMISHO KWA MWANAFUNZI MANISPAA YA KIGOMA UJIJI
1.Awe amesajiliwa shuleni na katika mfumo wa PREM.
2.Mwalimu mkuu wake amjazie fomu au awe amemjazia fomu za uhamisho , kusaini na kuzifunga vizuri.
3.Fomu zilizojazwa , kusainiwa na kugongwa mhuri wa mwalimu mkuu zipelekwe kwa mratibu elimu kata, asaini na kuzigonga mhuri.
4.Mzazi wa mwanafunzi azipeleke fomu zilizojazwa na mwalimu mkuu na mratibu elimu kata kwa afisa elimu wa wilaya.
5.Afisa elimu wa wilaya atafanya uhamisho wa mwanafunzi kwa njia ya kielektroniki(PREM) na kusaini nakala za uhamisho zilizotoka kwa mwalimu mkuu na mratibu elimu kata.
6.Mwanafunzi atapokelewa na afisa elimu wa wilaya aliyohamia kwa njia ya mfumo baada ya kupata namba za utambulisho wa mwaafunzi(PREM NUMBER) katika shule aliyohamia.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa