Na Mwandishi Wetu
Wadau mbalimbali Manispaa ya Kigoma/Ujiji Jana Februari 03, 2026 walianza mdahalo wa Siku mbili (02) ukilenga kuelimisha na kupinga vitendo vya ukatili katika jamii.
Mdahalo huo unafanyika katika ukumbi wa Ndela ukihuhudhuriwa na Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii, maafisa Ustawi wa Jamii, Viongozi wa dini, Watu maarufu, Vijana, Wazazi, na Walezi.
Akifungua mafunzo hayo Mratibu wa Dawati la Jinsia Manispaa ya Kigoma Ujiji Bi. Aida Nzowa aliwataka Wadau hao kuwa mabalozi na kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili katika jamii.
Alisema Manispaa hiyo imekuwa ikiathiriwa na vitendo vya ukatili kama vile Wazazi wa kiume kutelekeza familia zao na uwepo wa ndoa za utotoni.
Washiriki wa Mdahalo walijadili mbinu za kuzuia na kukabiliana na ukatili ikiwemo utoaji wa taarifa katika Mamlaka husika ikiwemo Ofisi za Mtaa, Kata, Ustawi wa Jamii, na Polisi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa