Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kutatua kero za Wananchi na kutekeleza miradi ya Maendeleo itakayoacha alama kwa Wananchi.
Ameyasema hayo Leo Januari 30, 2026 katika kikao alichokifanya na Waheshimiwa Madiwani katika ukumbi wa Manispaa hiyo kikihudhuriwa na Kamati ya ulinzi na Usalama Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo.
Amewataka kufanya kazi kwa Ushirikiano pamoja na Wataalamu katika usimamizi wa miradi, kusimamia na kubuni vyanzo vipya vya mapato.
Aidha amewataka kutenga fedha zitakosaidia kutekeleza miradi ya Maendeleo kwa Wananchi, na kusimamia Usafi wa mji katika Kata mbalimbali za Manispaa hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Mussa Maulidi amemhakikishia kiongozi huyo Baraza la Madiwani litaebdelea kusimamia miradi na maendeleo ya Wananchi, kubuni vyanzo vipya na kufanya kazi kwa umoja na Wataalamu waliopo.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa