Na Mwandishi Wetu
Shule ya Awali na Msingi Kagera iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji ni Miongoni mwa Shule kongwe zilizopo katika Manispaa hiyo ambapo ilianza Mwaka 1955.
Kwa Mwaka 2025, Shule ilipokea kiasi cha fedha za Kitanzania zaidi ya Millioni mia moja kumi na moja (Tsh 111,197,857.00/=) kutoka Serikali Kuu kwa lengo la ukarabati wa miundombinu iliyopo.
Ukarabati wa madarasa Manne (04) unaendelea kukamilishwa ambapo hadi sasa kiasi cha fedha za Kitanzania Millioni arobaini na nne (Tsh 44,000,000/=) zimeshatumika.
Aidha Serikali inaendelea na Ujenzi wa madarasa mengine manne (04) na matundu kumi na mbili (12) ya Vyoo kupitia Mradi wa BOOST kwa gharama ya fedha za Kitanzania Millioni Mia moja na arobaini (Tsh 140,000,000/=).
Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira ya utoaji elimu ili kuhakikisha wahitimu wanakuwa na maarifa na ujuzi stahiki na wenye uwezo wa kushindana Kimataifa.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa