Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ilipanga kutekeleza jumla ya miradi mitatu ya maji. Mradi wa maji wa Kibirizi (Group scheme), Mradi wa Maji wa Kagera na mradi wa Maji wa Mgumile.
Ujenzi wa Mradi wa Kagera (Buhanda na Businde) imeshakamilika na kukabidhiwa KUWASA kwa ajili ya kuunganishwa na bomba kuu litakaloingiza maji kwenye tenki
MRADI WA MAJI WA KIBIRIZI
Mradi huu umegharimu Tsh 325,095,920.00 (Mkataba wa awali kabla ya kusitishwa Tsh 1,092,945,590.00). Ulianza kujengwa tarehe 28.01.2013 na ulikuwa ukamilike tarehe 28.11.2013. Mkandarasi alikuwa D4N Co Ltd. – Kahama chini ya Usimamizi wa UWP Consulting Ltd – Dar es Salaam. Mradi ulikusudiwa kutoa huduma kwa watu 20,608 wa eneo la Kibirizi, Bushabani. Buronge na Mwasenga.
KAZI ZILIZOPANGWA KUFANYIKA KATIKA MRADI WA KIBIRIZI
Kujenga chanzo cha maji na kufunga pampu 2, Kujenga matenki 2 ya ujazo wa mita 225 (lita 225,000) na 135 (lita 135,000). Kujenga mtandao wa bomba wenye urefu wa kilometa 31. Kujenga magati 49 ya kuchotea maji. Kujenga nyumba ya mlinzi wa mitambo. Kujenga ofisi ya mradi.
KAZI ZILIZOFANYIKA
Ujenzi wa matenki ya ujazo wa mita 225 na 135 (Lita 225,000 & 135,000), ujenzi wa Magati ya maji 16 (hayajakamilika) kujenga mtandao wa bomba wa urefu wa kilometa 13. Ujenzi wa ofisi ya mradi ambayo imekamilika kwa 30%.
MRADI WA MAJI WA MGUMILE
Mkataba na mkandarasi wa ujenzi wa mradi huu ulisainiwa mwezi Aprili, 2014 lakini kukosekana kwa fedha kulisababisha kusimama utekelezaji wake.
Hivi sasa fedha kiasi cha Tsh 549,828,345.00 zimepatikana toka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na utekelezaji wa mradi huu umeanza mwezi Februari, 2017.
Mradi huu utagharimu Tsh 549,828,345.00. Umeanza kujengwa tarehe 16.02.2017 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30.07.2017. Mkandarasi ni Maginga Business Holdings Co Ltd. – Dodoma chini ya Usimamizi wa Mhandisi wa Maji wa Manispaa. Mradi umekusudiwa kutoa huduma kwa watu 2,795 wa Mtaa wa Mgumile.
KAZI ZILIZOPANGWA KUFANYIKA KATIKA MRADI WA MGUMILE
Kujenga chanzo cha maji na kufunga pampu 1, kuweka Solar panels, Kujenga tenki 1 la ujazo wa mita 80 (lita 80,000). Kujenga mtandao wa bomba wenye urefu wa kilometa 7.5. Kujenga magati 9 ya kuchotea maji. Kujenga nyumba ya mitambo. Kujenga ofisi ya mradi.
HALI HALISI YA SASA
Kazi iliyokwishafanyika mpaka kufikia tarehe 17.03.2017, imefikia asilimia 5.5 ya kazi yote.
CHANGAMOTO ZILIZOPO KWENYE UTOAJI WA HUDUMA YA MAJI
Utekelezaji wa Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira na utoaji wa huduma ya maji unakabiliwa na changamoto zifuatazo;
Ukosefu wa miundombinu ya barabara kwa ajili ya kufikisha vifaa vya ujenzi kwenye eneo la mradi wa Mgumile kwani eneo hili kwa sehemu kubwa limezungukwa na Ziwa na Mto Luiche. Kujaa kwa Mto Luiche kunasababisha pia eneo la barabara pekee isipitike na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa mradi.
Kuharibiwa kwa miundombinu iliyokamilika ujenzi wake katika mradi wa Kagera kabla ya kuanza kutoa huduma kutokana na kukaa muda mrefu.
Mamlaka ya Maji (KUWASA) kukosa fedha za kukamilisha ujenzi miradi iliyokabidhiwa kwao
MIKAKATI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa