Na Mwandishi
Mafunzo kwa Walimu wa Shule za Msingi Manispaa ya Kigoma/Ujiji wanaofundisha somo la Kiingereza kwa Wanafunzi wa darasa la Kwanza hadi la tatu yanaendelea Katika Shule ya Msingi Bushabani.
Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni Siku ya tatu (03) tangu kuanza ambapo yanatarajia kuhitimishwa Siku ya Kesho Alhamisi ya Februari 18, 2026 yakisimamiwa na Wataalamu kutoka Taasisi ya Elimu (TET) na kufadhiliwa na Mradi wa Shule Bora.
Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Mwalimu Hamis Rajabu Maundu amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo katika ufundisha wa somo la Kiingereza kwa kutumia mbinu mbalimbali za ujifunzaji na ufundishaji.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa