Na Mwandishi Wetu
Baraza la Madiwani Manispaa ya Kigoma/ Ujiji limejadili na kupitisha mpango na bajeti kiasi cha fedha za Kitanzania zaidi ya Billion arobaini na nne (Tsh 44,944,975,400/=) kwa Mwaka wa fedha 2026/2027
Baraza hilo limefanyika Leo Februari 17, 2026 likiongozwa na Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Mussa Maulidi na Kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali ikiwemo Kamati ya ulinzi na Usalama na Viongozi wa Vyama vya kisiasa.
Awali Akiwasilisha rasmu ya bajeti kwa niaba ya Mkurugenzi, Mchumi wa Manispaa hiyo Ndugu. Emmanuel Ntiboneka amesema kiasi hicho kinakisiwa kukusanywa kutoka mapato ya ndani zaidi ya bilioni tano (Tsh 5,985,756,400/=),matumizi ya kawaida yakiwa zaidi ya bilioni moja (Tsh 1,618,040,000/=) na fedha ya miradi Maendeleo ikiwa ni zaidi ya bilioni tisa (Tsh 9,673,767,000/=).
Amesema bajeti hiyo ina ongezeko la Mapato ya ndani zaidi ya milioni mia mbili (Tsh 223,960,400/=) sawa na asilimia moja (1%) ukilinganisha na bajeti ya fedha kwa mwaka 2025/2026.
Bajeti hiyo imetaja utekelezaji wa miradi ya Kimkakati yenye lengo la kuongeza Mapato ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Shule mpya ya English medium, na ujenzi wa maduka ya Kisasa na uwanja wa michezo Mwanga Community centre.
Aidha vipaumbele vya Halmashauri ni kuongeza mapato ya ndani na kuboresha huduma za jamii, kuongeza na kuboresha miundombinu ya huduma za jamii, Kuongeza tija katika shughuli za uzalishaji mali, Kuongeza ufanisi katika kushughulikia masuala mtambuka na uhifadhi wa mazingira kwa maendeleo ya kizazi cha sasa na kijacho.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa