Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amewataka Watumishi wa makao makuu ya Ofisi hiyo kukubali mabadiliko na kufanya kazi kidigitali kuendana na Kasi ya teknolojia.
Ameyasema hayo Leo Februari 16, 2026 katika mafunzo ya kidijitali ya mfumo wa ofisi mtandao (e-office management System) yaliyofanyikia katika ukumbi wa Manispaa hiyo yakiongozwa na Maafisa TEHAMA.
Amewataka Maafisa TEHAMA kuwawezesha Watumishi wote wanaingia na kufanya kazi kupitia mfumo ili kurahisisha mzunguko wa majalada ndani ya taasisi na kufanya maamuzi kwa wakati.
Mfumo wa E-Office unalenga kupunguza gharama, kurahisisha Mawasiliano na kukabiliana na changamoto ya kuhifadhi nyaraka kupitia Mawasiliano ya kidigitali.
ZAIDI BOFYA www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa