Na Mwandishi Wetu
Walimu wenye mahitaji maalumu Manispaa ya Kigoma/Ujiji wamekabidhiwa vifaa saidizi kwa lengo kuongeza ari na kukuza ufundishaji.
Vifaa hivyo kutoka Serikali Kuu vimekabidhiwa Leo Januari 30, 2026 na Afisa Elimu Elimu Maalumu Ndugu. Shingwa Hamis Shingwa ambapo amewataka kuvitumia katika kukuza ufaulu na ufundishaji kwa Wanafunzi.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Walimu Tisa (09) wa Shule za Sekondari na Msingi wenye ulemavu wa uoni, usikivu na ulemavu wa viungo na kukabidhiwa vifaa kompyuta mpakato (laptops), vifaa vya sauti (Digital Sound), Vishikwambi, Karatasi za maandishi ya nukta nundu, na vifaa vya kutembelea.
Ikumbukwe kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Profesa Adolf Mkenda, alizindua zoezi la ugawaji wa vifaa vya kielimu na vya saidizi kwa walimu, wakufunzi na walimu tarajali wenye ulemavu vyenye thamani ya shilingi bilioni 5.3 Nchini kote.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
@professoradolfmkenda @ortamisemi
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa