Na Mwandishi Wetu
Idara ya Elimu Sekondari Manispaa ya Kigoma/Ujiji kupitia Mradi wa Wezesha Binti unaofadhiliwa na taasisi ya Enabel imekabidhi vifaa vya michezo kwa Wakuu wa Shule za Sekondari tano(05) zinazotekeleza mradi huo.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa Leo Februari 06, 2026 na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa Ndugu. Abdul Utimbe ambapo amewataka Wakuu wa Shule kutumia vifaa hivyo kuinua viwango vya michezo Shuleni.
Mratibu wa mradi wa Wezesha Binti unaofadhiliwa na taasisi ya Enabel Manispaa ya Kigoma Ujiji Bi.Neema Bugemwe amesema Shule zilizokabidhiwa vifaa hivyo ni pamoja na Shule ya Sekondari Kitwe, Bushabani, Wakulima, Rubuga na kitongoni.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Mipira, sare za michezo, Gloves, sabuni, ndoo, beseni, magoli, Kinga za mikononi (gloves), na Mahema.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa