Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua amewataka Watumishi ambao ni ajira mpya Manispaa ya Kigoma/Ujiji kutumia lugha nzuri katika kuwahudumia Wananchi.
Ameyasema hayo Leo March 07, 2025 alipokuwa akifungua mafunzo kwa Watumishi hao ambao ni ajira mpya katika kada ya Watendaji wa Mtaa, Elimu Sekondari na Afya.
Amewataka kufanya kazi kwa weredi kwa kuzingatia misingi inayosimia maadili ya utumishi wa Umma.
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imepokea Wataalamu ajira mpya 112, Watendaji wa Mtaa wakiwa 10 Walimu Elimu Sekondari 35 na Wataalamu wa afya 67.
Katika Mafunzo hayo mada mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo kazi, Majukumu, Wajibu, Maadili, Stahiki na Mapambano dhidi ya Vitendo vya rushwa.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa