Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Awamu ya Sita Nchini Tanzania chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha Sekta ya Uvuvi Manispaa ya Kigoma/Ujiji ili kuongeza tija na kipato kwa Wavuvi.
Serikali kupitia Mradi wa TACTICS inaendelea na ujenzi wa Mwalo wa Katonga kwa lengo la kuboresha miundombinu ya Mwalo na Soko la mazao ya Uvuvi.
Katika kuhakikisha Wavuvi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wanafanya kazi katika mazingira salama Serikali imenunua boti kwa ajili ya doria na udhibiti wa Uvuvi haramu.
Aidha kumekuwa na ongezeko la Kampuni kumi (10) za uchakataji na usafirishaji wa mazao ya uvuvi kwenda nje ya Nchi na ongezeko la Wananchi kufuga Samaki Kisasa kwa njia ya mabwawa na vizimba na kufanya uwepo vizimba 16 na mabwawa 40 ya Watu binafsi.
Karibu Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane) Banda la Manispaa la Manispaa ya Kigoma/Ujiji yanayoendelea Kanda ya Magharibi Manispaa ya Tabora katika Viwanja vya Fatuma Mwasa.
Kauli mbiu ya Mwaka huu 2025 ni "Chagua Viongozi Bora kwa maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa