Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigoma Leo March 25, 2025 imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani katika Miradi ya Maendeleo Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Ziara hiyo imefanyika ikiongozwa na Mwenyekiti Ndugu. Ahmedi Mwilima ambapo mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo amepongeza kwa namna Serikali imeendelea kutoa fedha katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya huduma za Jamii kwa Wananchi.
Aidha amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelidhishwa na namna miradi ya maendeleo inavyotekelezwa na kusimamia ili kuwanufaisha Wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua amepongeza Viongozi hao huku akisema maelekezo na Ushauri walioupata katika miradi mbalimbali wataendelea kuufanyia kazi.
Miradi iliyokaguliwa na kutembelewa ni Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Ujenzi wa Bwalo Shule ya Sekondari Kasingirima, Kuanza kwa Majaribio ya Uchinjaji katika Machinjio ya Kisasa Ujiji, Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Burega, Ujenzi wa Soko la Mwanga na kukagua upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa