Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji inatarajia kuendesha zoezi la kitaifa la umezaji dawa (kinga tiba) kwa lengo la kudhibiti magonjwa ya Minyoo ya Tumbo na Kichocho kwa Watoto wenye Umri wa kwenda Shule kuanzia miaka 5 hadi miaka 14.
Yamesemwa hayo Leo Novemba 22, 2023 Katika kikao cha afya ya Msingi Wilaya (PHC) kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kikihudhuriwa na Wadau mbalimbali.
Akiwasilisha taarifa katika kikao hicho Mratibu wa Magonjwa yasiyo ambukizwa Bi. Stela Lukinisha amesema umezaji wa kinga tiba utafanyika Siku ya Ijumaa Novemba 24, 2023 katika Shule za Msingi kwa Watoto walioandikishwa Shule na wasioandikishwa.
Amesema kinga tiba itakayotumika ni Albendazole kwa minyoo tumbo na Praziquantel kwa ugonjwa wa kichocho.
Awali akifungua kikao Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Kali amewataka Wazazi na Walezi kutoa ushirikianao katika zoezi hilo na kuepukana na dhana potofu zinazoweza athiri zoezi hilo.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa