Na Mwandishi Wetu
Wazazi na Walezi wenye Watoto chini ya Umri wa miaka nane (08) wametakiwa kushiriki zoezi la chanjo ya ugonjwa wa Polio inayotarajiwa Kutolewa Septemba 21-24, 2023 Wilayani Kigoma
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamis Kali Leo Septemba 12, 2023 alipokuwa akihutubia Wajumbe wa Kikao cha Kamati ya afya ya Msingi (PHC) kilichofanyikia Ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Katika Kikao hicho Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja amewataka Wajumbe wa Kikao hicho kuendelea kutoa elimu kwa Wakazi wa Manispaa hiyo na kuwataka Wananchi kushiriki kikamilifu
Awali akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Utoaji Chanjo ya Polio Mganga Mkuu wa Manispaa Dr. Hashim Mvogogo amesema Chanjo hiyo inatolewa kwa watoto chini ya miaka minane ambao wako katika hatari ya kupata maambukizi ya Ugonjwa huo
Amesema Chanjo ya Ugonjwa wa Polio ni salama na itatolewa bure na Watoa huduma za afya nyumba kwa nyumba, Vituo vya kutolea huduma za afya na Mashuleni
Ugonjwa wa Polio husababisha kupooza, Ulemavu na kifo ambapo husababishwa kwa kutozingatia kanuni za usafi kwa kunywa maji au vyakula ambavyo vimechafuliwa na kinyesi kutoka kwa mtu mwenye virusi vya ugonjwa huo
Wilaya ya Kigoma inatarajia kutoa Chanjo kwa watoto 178, 253 ambapo Manispaa ya Kigoma/Ujiji Watoto 90, 993 wanatarajia kupata Chanjo na Watoto 87, 260 kwa Watoto wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa