Na Mwandishi Wetu
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma na sasa Mkuu wa Wilaya ya Longido Ndugu. Hamis Kali amewaaga Watumishi wa Wilaya ya Kigoma huku akiwataka kuendeleza ushirikiano na Viongozi katika kuwatumikia Wananchi.
Nasaha hizo amezitoa Leo Septemba 09, 2024 alipokuwa akitoa hotuba ya kuwaaga Wakuu wa idara na Vitengo wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma katika Ukumbi wa Manispaa.
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka Viongozi hao kuendelea kufanya kazi kwa upendo na umoja ikiwa ni pamoja na kusimamia maendeleo ya Wananchi kwa uaminifu ili kutimiza adhima ya Serikali ya awamu ya Sita.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuendelea kuaminiwa katika kuwahudumia Wananchi huku akimtaka kuendelea kufanya kazi kwa weredi kama ambavyo amekuwa akisimamia maendeleo ya Wananchi Wilayani Kigoma.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa