Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Hamis Kali ameendelea kutoa elimu ya Kuzingatia maadili na miiko ya Kitanzania na kuepuka Vitendo vya ukatili
Aliyasema hayo Jana April 17, 2023 alipokuwa akihutubia Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Mtaa wa Taifa Kata ya Rusimbi ambapo pia alisikiliza Kerò za Wananchi pamoja na kuzitatua
Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka Wazazi kuendelea kuwaelimisha Watoto Kuzingatia maadili sahihi na kuepuka Migogoro na ukatili ndani ya familia inayosababisha ongezeko la watoto wa mitaani
Aidha aliwataka Wananchi kuendelea kuhamasika kulima zao la Michikichi ya Kisasa kwa lengo la kuwa na uzalishaji mkubwa na wenye tija ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na familia
Alisema tayari ugawaji wa kadi za vitambulisho vya Taifa (NIDA) unafanyika kwa kila Kata kwa Wataalamu kupita kugawa kwa kuhirikiana na viongozi wa eneo husika
Naye Diwani wa Kata ya Rusimbi Mhe. Bakari Songoro akiishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa niaba ya Wananchi kwa Utekelezaji wa miradi alisema Serikali imekamilisha Ujenzi wa wodi ya Wazazi katika Zahanati ya Rusimbi kwa gharama ya Tsh 76, 765, 000/= na tayari inafanya kazi
Alisema Serikali imeboresha Ujenzi wa vyumba vya Madarasa matatu (03) Katika Shule ya Sekondari Rusimbi kwa gharama ya Tsh 60, 000, 000/= , Uboreshaji wa maabara ya Shule kwa gharama ya Tsh 20, 000, 000/= na ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Kipampa
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa