Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe ameshuhudia utiaji saini wa utekelezaji wa mkataba wa afua za lishe kati ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/ Ujiji na Watendaji kata kumi na tisa (19) wa Manispaa hiyo uliofanyika Leo Novemba 1, 2022 katika Ukumbi wa Manispaa hiyo
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka Watendaji Kata na Mitaa kusimamia utekelezaji wa afua za lishe katika maeneo yao ili kuhakikisha kunakuwa na jamii ýenye watu wenye afya njema kutokana na ulaji wa vyakula kwa usahihi
Amewataka Watendaji Kata hao kuhakikisha wanatoa elimu kwa Wananchi namna ya utumiaji wa vyakula vinavyopatikana katika Mazingira yao huku akiwataka kuhakikisha wanakagua ubora wa bidhaa za vyakula vinavyouzwa katika masoko na maduka yaliyopo katika maeneo yao
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athumani Msabila amewataka Watendaji Kata hao kuwasilisha kila robo utekelezaji wa afua za lishe katika jamii na watoto waliopo ili kuwa na Watu wenye akili timamu na uwezo wa kufanya kazi
awali Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Dr. Hashimu Mvogogo akiwasilisha taarifa amesema Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 robo ya kwanza (July- Septemba) Manispaa ya Kigoma/Ujiji tayari imetoa fedha za utelezaji wa afua za lishe kiasi cha Tsh 8, 578, 000, 000/= sawa na Tsh 1000/= iliyotengwa kwa kila mtoto
Ameendelea kusema shughuli zingine zilizotekelezwa ni pamoja na utambuzi na matibabu kwa watoto ishirini na mbili (22) wenye utapiamlo kati ya elfu kumi Mia saba sabini na tano ( 10775) waliopimwa na kupewa matibabu katika Hospitali ya Mawenì na Babtisti, Kaya 8209 kati ya kaya 8522 zilizokuwa na wajawazito na watoto wenye umri wa miaka mitano (05) walitembelewa na kupewa elimu ya lishe
Oktoba 26, 2022 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma CGF (Mstaafu) Thobias Adengenye aliongoza kikao cha tathimini za Utekelezaji wa Afua za lishe kwa Mkoa na kusaini Mkataba na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mkoa huo kilichofanyikia Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa kasulu
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa