Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamis Kali Leo Oktoba 20, 2023 amefanya kikao na Wajasiriamali na Wafanyabiashara waliopo eneo la Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO-KIGOMA) kwa lengo la kuwasikiliza huku akitatua kero walizokuwa wakipitia.
Katika kikao hicho kilichofanyikia katika Ofisi za SIDO-KIGOMA amewataka Wajasiriamali kuendelea kufanya kazi kwa utulivu huku akiagiza Uongozi wa taasisi hiyo kuendelea kubuni na kuboresha mazingira ya biashara katika eneo hilo.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ameunda Uongozi wa mpito wa kusimamia uundaji wa Katiba ya Jumuia mpya ya Wajasiriamali na Wafanyabiashara wa eneo hilo pamoja na kusimamia Uchaguzi wa viongozi wapya kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ameutaka uongozi wa SIDO-KIGOMA kuendelea kuboresha miundombinu kuwa rafiki kwa Wafanyabiashara na kuzingatia usafi wa mazingira huku akikagua Shughuli za Wajasiriamali wa eneo hilo.
Pia, Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja, Diwani wa Mwanga Kaskazini Mhe. Sharon Mashanya na baadhi ya Wakuu wa idara na Vitengo.
zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa