Na Mwandishi Wetu
Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Jana March 2, 2023 walipokea na kujadili taarifa kutoka Kwa Wakuu wa Taasisi za Serikali zilizopo Katika Manispaa hiyo
Wenyeviti Walikutana katika Ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Katika kikao kilichoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Kali kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi katika maeneo yao ya Utawala
Katika kikao hicho Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka Wakuu wa Taasisi, Watendaji wa Serikali na Wenyeviti wa Serikali Mitaa kuwa na ushirikiano katika miradi inayotekelezwa ili kuhakikisha mafanikio ya kusogeza huduma za jamii karibu na Wananchi yanafikiwa
Aidha amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wakishirikiana na Watendaji wa Mitaa kusimamia suala la Usafi wa Mji kuanzia katika Makazi ya Watu na katika maeneo ya Umma
Mkuu huyo alisema amepanga kufanya mikutano ya hadhara na Wananchi kwa kila Kata akiwa pamoja na Wataalamu mbalimbali wa Idara za Serikali
Katika kikao hicho Wakuu mbalimbali wa Taasisi walitoa taarifa za Utendaji kazi ikiwemo Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Tanroads, Tarura, Tanesco, Mamlaka ya Maji (KUWASA), pamoja na Bandari
Kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kigoma, Mbunge, Meya, Naibu Meya na Wakuu wa idara na Vitengo Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa