Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua Leo March 26, 2025 amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha Julai 2024 hadi March 2025 kwa Halmashauri Kuu ya chama hicho Kigoma Mjini.
Akiwasilisha taarifa hiyo katika kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndugu. Ahmedi Mwilima amesema Serikali imetekeleza miradi mbalimbali ikiwa na lengo la kuboresha huduma za jamii, Maendeleo ya Miundombinu na ukuaji wa Uchumi kwa Wananchi.
Amesema katika Sekta ya elimu Ujenzi wa vyumba vya madarasa umeongezeka, Ongezeko la Madawati kutoka 9791 hadi 10,066, na Ujenzi wa Shule Mpya za Sekondari Kata ya Kipampa na Buzebazeba.
Aidha Vikundi 23 vya Wajasiriamali vimesajiliwa huku mikopo ya vikundi vya Wanawake, Vijana na Walemavu ikitolewa kiasi cha Tsh 273,366,601.30 na tayari Marejesho yanaendelea.
Akiendelea kuwasilisha amesema hati 600 za umiliki wa ardhi zimetolewa kwa Wananchi, Viwanja 852 vimepimwa kwa mpango shirikishi huku upanuzi wa njia ya kurukia na kutua ndege na uboreshaji wa miundombinu ya Uwanja wa ndege wa Kigoma ukiwa unaendelea.
Amehitimisha kwa kusema Serikali kupitia Kampuni ya meli ya Tanzania (TASHICO) imetekeleza miradi ya ujenzi wa meli Mpya mbili (Roro na Wagon Ferry) za kubeba mizigo, Ukarabati wa Meli tatu (MV Sangara, MV Liemba, na MV Mwongozo) na Ujenzi wa kiwanda cha kujenga meli.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa