Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua Leo Septemba 03, 2025 amefanya ziara ya kukagua miradi inayotarajiwa kutembelewa, kukaguliwa, Kuzinduliwa na kuwekewa jiwe la Msingi katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Kiongozi huyo amefanya ziara akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Akiwa katika ziara hiyo amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi September 21, katika eneo la Mapokezi Shule ya Sekondari Buronge, Maeneo ya miradi pamoja na eneo Mkesha ambalo ni Mwanga community centre.
Mkuu huyo wa Wilaya amekagua ujenzi wa bweni Shule ya Sekondari Buronge, Ujenzi wa Zahanati ya Rubuga, Ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kasimbu, Ujenzi wa barabara ya Met na kukagua Shughuli za Kikundi cha Vijana cha umoja wa mafundi Seremala Katubuka pamoja na Ujenzi wa KG One Hotel.
Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Kigoma/Ujiji unatarajiwa kukimbizwa Septemba 21, Mwaka huu.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz #mwengewauhuru #mwengewauhuru2025
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa