Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imepokea Watumishi wapya zaidi ya Mia moja (100) katika kada mbalimbali kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Hayo yameelezwa Leo Februari 11, 2026 na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba wakati akifungua kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichokuwa na lengo la kujadili rasimu ya mpango na bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kilichofanyika katika ukumbi Manispaa hiyo.
Kikao hicho kimefanyika kikihudhuriwa na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi, Wakuu wa Idara na Vitengo huku Mkurugenzi huyo akiwataka Viongozi hao kuwasaidia Watumishi wapya kuwaelekeza namna bora katika kuwahudumia Wananchi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa